Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Palestina yakataa mazungumzo na Marekani

media Sintofahamu yaibuka katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi baada ya kutokea makabiliano kati ya waandamanaji na askari wa Israel. REUTERS / Mohamad Torokman

Mamlaka ya Palestina imekataa mazungumzo yoyote na Marekani na kusema kuwa Marekani imejishusha hadhi yake duniani. Kauli hiyo inakuja siku mbili baada ya rais wa Marekabi Donald Trump kuchukua uamuzi wa kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Hata hivyo Marekani imeionya Palestina dhidi ya uamuzi huo kutotaka kukutana na makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika mapema mwezi huu ili kujadili uamuzi wa rais Trump wa kuhamishia Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Makamu wa rais wa Marekani anajianda kuzuru ukanda wa Mashariki ya Kati lakini kiongozi wa ngazi za juu wa Palestina, Jibril Rjoub amesema kuwa kiongozi huyo hakaribishwi Palestina, na kumuonya kutothubutu kwenda Palestina kwani “ataaibika”.

Hatua hii ya Palestina imewaweka mashakani viongozi wa Marekani, huku Marekani ikiisihi Palestina kutengua hatua hiyo.

Ikulu ya Marekani imesema, uamuzi huo uliofikiwa na Palestina utakuwa hauna maana kwa kuwa hawataweza kupata suhulu ya mgogoro huo. Hatua hiyo imekuja mapema baada ya rais Trump kutangaza kuwa anautambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Hayo yanajiri wakati ambapo makabiliano kati ya Wapalestina na polisi ya Israel yanaendelea. Mpaka sasa inaarifiwa kuwa Takriban Wapalestina 31 wamejeruhiwa katika makabiliano yaliyozuka Ukanda wa Gaza na maeneo ya Ukingo wa Magharibi yanayotawaliwa na Israel.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana