Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAEL-MAREANI-USALAMA

Hali ya sintofahamu yaendelea Palestina kufuatia uamuzi wa Trump kuhusu Jerusalem

Hatua ya rais wa Marekani Donald Trump kutambua Jerusalem kuwa mji Mkuu wa Israel na kutangaza kuhamisha ubalozi wa wa nchi hiyo kutoka Tel Aviv, imeanza kuzua makabiliano kati ya waandamani wa Kipalestina na maafisa wa usalama wa Israel.

Vijana wenye hasira wameonekana wakiwasha matairi moto na kuwarushia mawe, maafisa wa usalama wa Israel katika mji wa Bethlehem.
Vijana wenye hasira wameonekana wakiwasha matairi moto na kuwarushia mawe, maafisa wa usalama wa Israel katika mji wa Bethlehem. REUTERS/Mohamad Torokman
Matangazo ya kibiashara

Vijana wenye hasira wameonekana wakiwasha matairi moto na kuwarushia mawe, maafisa wa usalama wa Israel katika mji wa Bethlehem.

Maafisa wa Israel walilazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kujaribu kuwasambaratisha kundi la vijana waliokuwa wanawarushia mawe.

Baada ya Trump kutangaza hatua hiyo, uongozi wa Palestina uliitisha maandamano makubwa kwa kipindi cha siku tatu kuanzia siku ya Jumatano kupinga hatua hiyo.

Maandamano makubwa yanatarajiwa leo mjini Ramallah na maeneo mengine ya Palestina, baada ya maombi ya Ijumaa, kupinga hatua hiyo ya Marekani.

Israel imetuma wanajeshi wake katika mpaka na Palestna kuhakikisha kuna inakabiliana na maandamano yoyote yatakayolenga kuwaumiza raia wa nchi yao.

Mbali na hilo, leo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana leo katika kikao cha dharura kujadili na kuthamini hatua hii ya Marekani ambayo imekosolewa na mataifa mengi duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.