Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Hatua ya Trump kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel yakosolewa kimataifa

media Donald Trump akionyesha tangazo rasmi ambapo Marekani inatambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka katika eneo la sasa la Tel Aviv kwenda Jerusalem. Haya ni maamuzi ya kihistoria yanayobadili sera za miaka mingi za Marekani kwa kuutambua mji wa Jerusalem kuwa ndio mji mkuu wa Israel.

Bw Trumpa amesema “uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za kuleta amani katika eneo hilo la mashariki ya kati”.

Tayari hatua hii imekosolewa kimataifa na kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kimeitishwa kesho Ijumaa.

- UFARANSA

"Ni uamuzi mbaya ambao Ufaransa haukubali, na unakiuka sheria za kimataifa na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Mji wa Jerusalem ni suala la usalama wa kimataifa, na nataka kufafanua mbele yenu kuwa suala la mji wa Jerusalemu linatakiwa kuamuliwa na Waisraeli na Wapalestina wenyewe katika mazungumzo chini ya Umoja wa Mataifa. Napenda kuwakumbusha nia ya Ufaransa na Ulaya katika ufumbuzi wa mataifa haya mawili, Israeli na Palestina zinatakiwa kuishi kwa pamoja kwa amani na usalama katika mipaka inyaotambuliwa kimataifa na Jerusalem kama mji mkuu wa mataifa haya mawili. Ninatoa wito kwa utulivu, amani, na jukumu kwa wote. Tunapaswa kuepuka vurugu kwa gharama zote na kuyapa kipaumbele mazungumzo, "Emmanuel Macron amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Algiers, mji mkuuwa Algeria ambako anazuru.

- HAMAS

Kwa upande wa chama cha Hamas, uamuzi wa rais wa Marekani unafungua "milango ya vita dhidi mali ya Marekani katika kanda hii." Ismail Radwan, afisa mwandamizi wa Hamas akizungumza na waandishi wa habari katika Ukanda wa Gaza, alitoa wito kwa nchi za Kiarabu na Waislamu "kusitisha mahusiano ya kiuchumi na kisiasa" na balozi za Marekani, na kuwatimua mabalozi wa Marekani.

Siku tatu za maandamano ya hasira katika maeneo ya Palestina

- PLO

Katibu Mkuu wa chama cha Mahamoud Abbas, PLO, Saeb Erekat, ametangaza kwa upande wake kwamba Donald Trump "ameharibu" ufumbuzi wa wmataifa mawili kwa kutangaza kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli. Kwa maoni yake, rais wa Marekani pia "ameididimiza Marekani kwa mchango wake katika mchakato wowote wa amani." "Kwa maamuzi haya mabaya. Marekani imedhoofisha juhudi zote za amani kwa makusudi na inatangaza kuwa inaachana na jukumu la kufadhili mchakato wa amani iliochangia katika miongo ya hivi karibuni," rais wa Palestina Mahmoud Abbas alisem akwenye runinga ya Palestina. Jerusalem ni "mji mkuu wa milele wa nchi ya Palestina," aliongeza.

Makundi mbalimbali ya Palestina wametoa wito wa "siku tatu za hasira". Katika Ukanda wa Gaza, mamia ya Wapalestina wenye hasira walichoma moto bendera za Marekani na Israeli na picha za Donald Trump. Maandamano makubwa yamepangwa kufanyika leo Alhamisi katika mji wa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi, eneolinalodhibitiwa na jeshi la Israel kwa miaka 50.

- SAUDI ARABIA

Saudi Arabia imesikitishwa na uamuzi wa siku ya Jumatano usiku "uamuzi usio na haki na usioeleweka" wa Donald Trump kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli. Katika taarifa, Saudi Arabia inasema ilionya kutokea "madhara ya hatari" ambayo yatasababishwa na kuhamisha ubalozi wa Marekani Jerusalem.

- JORDAN

"Uamuzi wa Rais wa Marekani kutambua Jerusalemu kama mji mkuu wa Israel, na kuhamisha ubalozi wa Marekani katika mji huo, ni ukiukwaji wa maamuzi ya sheria ya kimataifa na mkataba wa Umoja wa Mataifa," msemaji wa serikali ya Jordan, Mohammed Moumeni, alisema katika taarifa yake.

- UMOJA WA MATAIFA

Katika hotuba ambayo ilidumu dakika zisizozidi mbili na ambapo jina la Donald Trump halikutamkwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani uamuzi wa rais wa Marekani. "Toka nichukuwe hatamu ya uongozi kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, nimekua nikipinga hatua yoyote ya nchi ambayo ingeweza kuathiri matarajio ya amani kwa Waisrael na Wapalestina. Hali ya Jerusalem inapaswa kutatuliwa kupitia mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili kwa misingi ya maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Mkutano Mkuu, kwa kuzingatia masuala halali kutoka Palestina na Israeli, "Guterres amesema.

Donald Trump akisaini ubalozi wa Marekani kuhamishwa Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli, DESEMBA 6, 2017. REUTERS/Kevin Lamarque

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana