Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kuhusu uamuzi wa Trump

media Jumuiya ya kimataifa imeendelea kukosoa uamuzi wa rais wa Marekani kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel. REUTERS/Eduardo Munoz

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana siku ya Ijumaa Desemba 8 kwa ombi la mataifa nane ili kujadili uamuzi wa Donald Trump kutambua Jerusalemu kama mji mkuu wa Israeli, wanadiplomasia walmehakikishi taarifa hiyo siku ya Jumatano usiku.

Ombi hilo liliwasiliswa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Ufaransa, Bolivia, Misri, Italia, Senegal, Sweden, Uingereza na Uruguay.

"Umoja wa Mataifa uliipa Jerusalem jukumu la kisheria na kisiasa, ambalo Baraza la Usalama litoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuliheshimu. Ndiyo sababu tunaamini kwamba Baraza la Usalam la Umoja wa Mataifa linapaswa kushughulikia suala hilo haraka," Antonio Naibu balozi wa Sweden katika Umoja wa Mataifa, Carl Skau, alisema.

Mkutano hu, utafanyika mwishoni kesho Ijumaa mchana, saa za New York, ujumbe wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa umebaini.

Katika azimio lake la 2334, lililopitishwa mnamo mwezi Desemba 2016 kwa kura 14 dhidi ya kura moja ya utawala wa Barack Obama, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa "linasisitiza kuwa halitatambua mabadiliko yoyote katika mipaka iliyowekwa tarehe 4 Juni 1967, ikiwa ni pamoja na kesi ya Jerusalem, isipokuwa kama kutatokea makubaliano katika ya pande husika kupitia mazungumzo ".

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana