Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Onyo zaendelea kutolewa kabla ya uamuzi wa Trump kuhusu Jerusalem

media Ubalozi wa Marekani Tel Aviv. JACK GUEZ / AFP

Rais wa Marekani Dnald trump anaendelea kukabiliwa na vitisho vya kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia wa nchi hiyo na jumuiya ya nchi za Kiarabu kufuatia nia yake ya kutaka kuhamishia ubalozi wa Marekani nchini Israel katika mji wa Jerusalem kutoka mji wa Tel Aviv.

Kama kweli atachukua uamuzi huo kama alivyomtaarifu kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas na Mfalme wa Jordan au kuutambua mji huo mtakatifu kama mji mkuu wa Israel, Donald Trump atakua amekwenda kinyume na msimamo wa jumuiya ya kimataifa na viongozi wengi waliomtangulia katika uongozi wa taifa la Marekani. Nchi za Kiarabu zimeendelea kutoa onyo kufuatia hatua hiyo ya Marekani.

Ikulu ya White House imethibitisha kuwa rais Donald Trump atazungumza leo Jumatano kuhusu uwezekano wa kuhamishia ubalozi wa Marekani Jerusalem.

Kwa mujibu wa msemaji wa ikulu ya white house Sarah Sanders amesema kuwa Trump alizungumza na baadhi ya viongozi siku ya jumanne kuhusu mpango wake ya kuhamishia ubalozi huo kutoka tel aviv kuupeka Jerusalem.

Viongozi wa Palestina, Misri, Jordan na saudi arabia, wametoa onyo kwa rais Trump kuwa kuhamishia ubalozi huo Jerusalem kutadhoofisha kabisa juhudi za kuleta amani Mashariki ya Kati.

Siku ya Jumanne rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema kuwa ana wasiwasi kuwa rais huyo wa Marekani anaweza kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Israel na Palestina wote wanadai kuwa mji huo ni mji wao mkuu.

Israeli ilivamia eneo hilo la Mashariki mwa Palestina mwaka 1967 na kulifanya kama eneo lake baadae. Uamuzi huu hautambuliwi kimataifa. Israeli inaona mji huo kuwa mji wake mkuu.

Kwa upande wao, Wapalestina wanadai Jerusalem ya Mashariki kama mji wao mkuu wa baadae.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana