Pata taarifa kuu

Trump kutangaza uwezekano wa kuhamisha ubalozi wa Marekani Jerusalem

Rais wa Marekani Donald Trump atatangaza "siku zijazo" uamuzi wake kuhusu uwezekano wa kuhamishwa kama ahadi ya kampeni yake katika uchaguzi wa urais, ubalozi wa Marekani nchini Israeli kutoka Tel Aviv kuhamishiwa Jerusalem, msemaji wa White House.

Mji wa jerusalem, Israel, Septemba 23, 2016.
Mji wa jerusalem, Israel, Septemba 23, 2016. Mekudeshet
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, maafisa waandamizi wa Marekani wamesema kuwa Donald Trump atatoa hotuba siku ya Jumatano ambapo anaweza kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli, uamuzi unaokwenda kinyume na msimamo ulioshuhudiwa kwa miaka mingi na Marekani na ambao unaweza kuchochea mvutano katika Mashariki ya Kati.

Wakati huo huo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemuambia Donald Trump kuwa ana wasiwasi kuwa rais huyo wa Marekani anaweza kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Uamuzi wowote kuwa mji huo unastahili kuwa katika viwango vya mazungumzo kati ya Israel na Palestina, raisMacron amesema.

Israel na Palestina wote wanadai kuwa mji huo ni mji wao mkuu.

Israeli ilivamia eneo hilo la Mashariki mwa Palestina mwaka 1967 na kulifanya kama eneo lake baadae. Uamuzi huu hautambuliwi kimataifa. Israeli inaona mji huo kuwa mji wake mkuu.

Kwa upande wao, Wapalestina wanadai Jerusalem ya Mashariki kama mji wao mkuu wa baadae.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.