Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Kifo cha Ali Abdullah Saleh chauzua wasiwasi Yemen

Kuuawa kwa rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh, kumezua wasiwasi wa hali ya usalama wa nchi hiyo ambayo imeendelea kuwa katika hali ya kivita.

Rais wa zamani wa Yemeni Ali Abdallah Saleh, hapa ilikua Aprili 22, 2011, Sanaa.
Rais wa zamani wa Yemeni Ali Abdallah Saleh, hapa ilikua Aprili 22, 2011, Sanaa. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa zamani aliuawa jana na waasi wa Kihuthi ambao zamani walikuwa wanamuunga mkono.

Ripoti zinasema kuwa, Saleh alishambuliwa akiwa na gari lake wakati waasi hao wa Kihuthi walipokuwa wanapambana na kikosi kinachoongozwa na Saudi Arabia.

Waasi wa Kihuthi wamesema ndio waliomuua rais huyo wa zamani kwa kosa la uhaini.

Siku chache zilizopita, Saleh alisema alikuwa tayari kuzungumza na jeshi linaloongozwa na Saudi Arabia na kumaliza vita ambavyo vimekuwa vikiendelea tangu mwaka 2015.

Ali Abdullah Saleh, aliongoza Yemen kwa zaidi ya miaka 30 kabla ya kuzuka kwa vita vya kumwondoa madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.