Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh auawa Sanaa

Waasi wa Houthi nchini Yemen wanasema rais wa zamani wa nchi hiyo Ali Abdullah Saleh aliuawa katika vita katika mji mkuu wa Sana'a. Habari hii imethibitisha masaa machache baadaye na kiongozi wa chama cha rais wa zamani wa nchi hiyo.

Rais wa zamani wa Yemen, Ali Abdullah Saleh, (hapa ilikua mnamo mwezi Agosti 2017).
Rais wa zamani wa Yemen, Ali Abdullah Saleh, (hapa ilikua mnamo mwezi Agosti 2017). REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Waasi wa Houthis walikuwa katia mgogoro na kiongozi wa zamani wa Yemen, ambaye alikuwa aliungana na Saudi Arabia wiki iliyopita. Rais wa Yemeni Abd Rabbo Mansour Hadi ameamuru askari wake kuweka kwenye himaya yao mji mkuu Sanaa.

Kituo cha televisheni Al-Massira kilitangazataarifa ya kifo cha aliyekuwa Rais Ali Abdullah Saleh wakati wa mapigano katika mji mkuu Sanaa, kwa maneno haya: "Wizara ya Mambo ya Ndani (inayodhibitiwa na waasi) inatangaza mwisho wa kundi la wanamgambo wa waasi na kifo cha kiongozi wake (Ali Abdullah Saleh) na wahalifu wengine kadhaa. ".

Picha na video zinazunguka kwenye mitandao ya kijamii. Picha hizi zilipigwa tu kabla ya tangazo la waasi wa Houthis.

Picha na video zilizosambazwa mtandaoni zimeuonesha mwili wa mwanamume anayefanana na Bw Saleh ukiwa na kidonda kichwani.

Siku ya Jumamosi, Bw Saleh aliahidi "kufungua ukurasa mpya" na Bw Hadi anayesaidiwa na muungano wa mataifa yanayoongozwa na Saudi Arabia iwapo majeshi hayo yangeacha kuishambulia Yemen na kuondoa marufuku ya kutoingiza chakula na bidhaa Yemen.

Mzozo huo pamoja na marufuku ya kutoingiza chakula na bidhaa Yemen ambayo imekuwa ikitekelezwa na Saudi Arabia pia umewaacha watu 20.7 milioni wakihitaji kwa dharura msaada wa kibinadamu, na pia kusababisha hitaji kubwa zaidi ya chakula cha dharura duniani.

Kiongozi wa chama cha rais wa zamani Ali Abdullah Saleh, General People's Congress (CPG) kimethibitisha taarifa hii masaa machache baadaye kwa sirika la habari la AFP. "Aliuawa kama shujaa wakatiakipigania taifa," alisema kiongozi huyo wa chama, akilituhumu kundi la waasi la Houthi kuhusika na mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.