Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Wapalestina waanza mazungumzo ya kuboresha maridhiano Cairo

media Wapalestina waingia mitaa, Aprili 29 huko Gaza kwa kudai hasa kusitishwa kwa uhasama kati ya Hamas na Fatah. AFP PHOTO / MOHAMMED ABED

Makundi makuu ya Wapalestina, ikiwa ni pamoja na Hamas na Fatah, wameanza leo Jumanne mjini Cairo mazungumzo mapya yenye lengo la kuboresha maridhiano, licha ya kuendelea kwa tofauti kubwa.

Jameel Mezher, afisa mwandamizi kutoka vugu vugu la PFLP, amelithibitishia shirika la habari la AFP muda mfupi kabla ya mchana kuwa mazungumzo yameanza, bila kutoa maelezo zaidi.

Mkutano, uliopangwa kwa siku tatu, unafanyika katika makao makuu ya idara ya ujasusi ya Misri, ambayo inasimamia mazungumzo.

Tangu makubaliano yaliyofikiwa mwezi uliopita chini ya kivuli cha Misri, mvutano umeibuka kati ya Mamlaka ya Palestina inayoongozwa na Mahmaoud Abbas-kutoka chama cha Fatah na kundi la Kiislamu la Hamas.

Baada ya miaka kumi uhasama, makundi haya mawili hasimu yalikubaliana Oktoba 12 kuwa Hamas kukabidhi Mamlaka ya Wapalestina, Desemba 1, mamlaka katika Ukanda wa Gaza inayodhibiti.

Hamas ilitimua Mamlaka Palestina katika eneo la Gaza katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2007. Tangu wakati huo, Mamlaka ya Palestina haina utawala wowote katika eneo hilo, pamoja na vikwazo vilivyowekwa na Wayahudi, kwenye mashamba ya Ukingo wa Magharibi, mbali kidogo na Gaza.

- Hofu ya mgogoro mwingine kuzuka-

Kwa upande wake, Umoja wa Mataifa unataka kuamini kwamba kwa kukabidhi eneo la Gaza kwa Mamlaka ya Palestina, Wapalestina watasaidia kupatikana kwa suluhui katika mojawapo ya migogoro ya zamani zaidi duniani.

"Hatuna haki ya kuruhusu mchakato huu kushindwa, na ikiwa ni hivyo, hali hiyo inaweza kusababisha mgogoro mwingine mbaya zaidi," mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Nickolay Mladenov ameonya.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana