Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Urusi: mwafaka utapatikana katika maungumzo ya amani Syria

Mazungumzo mapya ya amani kujaribu kumaliza mzozo nchini Syria yalianza siku ya Jumatatu jijini Astana nchini Kazakhstan. Lakini makundi mengine kama vile Islamic State haikuhusishwa katika mazungumzo hayo.

Mazungumzo ya amani Astana kuhusu Syria yanaendelea, na Urusi inasema ina imani kuwa yatazaa matunda.
Mazungumzo ya amani Astana kuhusu Syria yanaendelea, na Urusi inasema ina imani kuwa yatazaa matunda. REUTERS/Mukhtar Kholdorbekov
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya, yanaongozwa na Urusi ambayo imekuwa mshirika wa karibu wa Rais Bashar Al Assad, baada ya kuanza kuliunga mkono jeshi la Syria mwaka 2015.

Urusi inasema ina uhakika mwafaka utapatikana katika mazungumzo haya kati ya serikali ya Damascus na upinzani na kumaliza vita vya miaka sita.

Mazungumzo kama haya yaliyofanyika hapo awali hayakuzaa matunda yoyote.

Vita nchini Syria vimesababisha vifo vya watu wengi na mamia kwa maelfu kulazimika kukimbilia nchi jirani na wengine kujaribu kuvuka bahari kuelekea Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.