Pata taarifa kuu
IRAQ-IS-USALAMA

Iraq yaendesha mashambulizi kabambe dhidi ya ngome ya mwisho ya IS

Iraq imezindua Alhamisi hii mashambulizi makubwa dhidi ya ngome ya mwisho ya kundi la Islamic State (IS) katika nchi hiyo karibu na mpaka na Syria, nchi ambayo wapiganaji wa kundi hilo wamekua wakikabiliwa dhidi ya vikosi vya serikali ya Damascus na wapiganaji wa Kikurdi wanaosadiwa na Marekani.

Majeshi ya Iraq karibu na mji wa Akashat, katika mkoa wa Anbar, Septemba 15, 2017.
Majeshi ya Iraq karibu na mji wa Akashat, katika mkoa wa Anbar, Septemba 15, 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

Vita hivi vinavyoshuhudiwa pande zote mbili za mpaka wa Iraq na Syria, "ni vita vikubwa vya mwisho dhidi ya kundi la IS", maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Marekani walisema hivi karibuni. Vita hivi vinalenga kuwatimua na kuwasambaratisha wapiganaji wa IS kutoka eneo lenye bonde la mkoa wa Deir Ezzor mashariki mwa Syria hadi Al-Qaim, magharibi mwa Iraq.

Ni katika eneo hili la jimbo kubwa la jangwa la al-Anbar ambako vikosi vya Iraq vimezindua Alhamisi hii asubuhi mashambulizi kabambe.

Alfajiri, Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi, Amiri mkuu wa majeshi, alitangaza katika taarifa yake "uzinduzi wa vita vya ukombozi wa al-Qaim."

Bw. Abadi, ambaye mara kadhaa alitangaza mashambulizi wakati wa hotuba ya televisheni usiku wa manane, wakati huu ametoa taarifa, kwani yuko katika ziara ya kikanda, ambaye baada ya eneo la Ghuba mwishoni mwa wiki iliyopita, alizuru Amman na Cairo kabla ya Ankara siku ya Jumatano, na leo Alhamisi anatahitimisha ziara yake nchini Iran.

Atakutana wakati wa mchana na Rais Hassan Rohani na Kiongozi Mkuu Ali Khamenei, viongozi wawili wakuu ambao ni jirani wakubwa wa Iraq.

Mnamo mwaka 2014, wapiganaji wa IS waliteka maeneo mengi karibu theluthi moja ya Iraq, lakini tangu wakati huo vikosi vya serikali na wanamgambo wa Iraq wamewatimua kwa zaidi ya 90% ya eneo lao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.