Pata taarifa kuu
IRAN-HAKI

Iran yamhukumu kifo raia wa Israel kwa ujasusi

Nchini Iran, mahakama imemhukumu kifo raia wa Israel mwenye asili ya Iran, ikimshtumu kufanya ujasusi kwa niaba ya Israel. Hata hivyo duru zisizo rasmi zinasema kuwa daktari Ahmadreza Djalali ni raia wa Sweden mwenye asili ya Iran.

Rais wa Iran Hassan Rohani, Septemba 22 2017.
Rais wa Iran Hassan Rohani, Septemba 22 2017. President.ir/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa mashtaka nchini Iran Tehran Abbs Jafari-Dowlatabadi, alisema Ahmadreza Djalali alipatikana na hatia ya kuwapasha habari majasusi wa Israel kuhusu anuani 30 za wanasayansi wa nyuklia, wawili kati yao waliouawa kwenye mashambulizi ya mabomu mwaka 2010.

Bw. Jafari-Dowlatabadi amesema kuwa anuani hizo ni za wanasayansi wa nyuklia Massoud Ali-Mohammadi na Majid Shahriari, ambao waliuawa kwenye milipuko ya mabomu mjini Tehran mwezi Januari na Novemba mwaka 2010.

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International limebaini kwamba daktari Ahmadreza Djalali alifanyiwa mateso sehemu alipokua akizuiliwa kabla ya hukumu hiyo isiyo ya haki.

Daktari Djalali anasema kuwa wakati akiwa kizuizini alilazimishwa mara mbili kukiri mbele ya kamera kwa kusoma taarifa zilizokuwa zimeandikwa na wale walikuwa wakimhoji.

Amesema alikuwa chini ya shinikizo kali kupitia mateso ya kisaskolojia na vitisho vya kumuua na kuwakamata watoto wake ili aweze kukiri kuifanyia ujasusi serikali ya Israel.

Amnesty International inasema kuwa daktari Djalali ni muadhiri kwenye taasisi ya Karolinska mjini Stockholm, alikuwa kwenye ziara ya kibishara nchini Iran mwezi Aprili mwaka 2016, wakati alikamatwa na maafisa wa ujasusi na kuzuiliwa bila ya kuruhusiwa kukutana na wakili kwa muda wa miezi saba.

Amnesty International imelaani hukumu hiyo ikisema kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea nchini Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.