Pata taarifa kuu
UTURUKI, SYRIA-USALAMA

Jeshi la Syria lazingira ngome za mwisho za kundi la IS

Jeshi la serikali ya Syria linaendelea kuziteka ngome za kundi la Islamic State. Siku ya alhamisi jeshi la Syria pamoja na washirika wake walifaulu kuzingira mji wa al-Mayadeen, mojawapo ya miji miwili ambayo iko mikononi mwa kundi la Islamic Sate katika mkoa wa mashariki wa Deir Ezzor.

Wapiganaji wa serikali ya Syria karibu na mkoa wa Deir Ezzor, Septemba 6, 2017 (picha ya zamani).
Wapiganaji wa serikali ya Syria karibu na mkoa wa Deir Ezzor, Septemba 6, 2017 (picha ya zamani). George OURFALIAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Syria na washirika wake,wakisaidiwa na jeshi la anga la Urusi, siku ya alhamisi waliweza kudhibiti barabara inayounganisha mji wa al-Mayadeen na mji wa Bou Kamal, kilomita 85 zaidi kusini mwa Syria, kwenye mpaka na Iraq. Hii ni miji miwili ya mwisho ambayo bado inashikiliwa na kundi la Islamic Sate nchini Syria.

Mji wa al-Mayadeen, kutoka kilomita 45 kusini mwa Deir Ezzor, kwa sasa umezingirwa na askari wa serikali, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) na vyanzo vilivyo karibu na serikali ya Damascus.

Al-Mayadeen ni mojawapo ya ngome muhimu zaidi ya kundi la Islamic State.

Wakati huo huo majeshi ya Uturuki yanaendelea na operesheni nchini Syria.

Vikosi vya majeshi ya Uturuki vimesonga mbele katika operesheni ya kijeshi nchini Syria kutokomeza wapiganaji wa jimbo la Idlib.

Magari ya Uturuki yameonekana yakisindikizwa na makundi ya wapiganaji wanaoungwa mkono na Al Qaeda katika jimbo la Idlib, huku kundi la Tahrir al-Sham likimili maeneo karibu na kambi ya majeshi ya Kikurdi ambayo yanapigana dhidi ya IS.

Operesheni hiyo iliyonza siku ya jumamosi inajumuisha majeshi ya Uturuki na yale ya Syria.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema hatavumilia vitendo vyovyote vya kigaidi katika eneo lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.