Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 26/06 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 26/06 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 25/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Ufaransa: Mbunge Agnes Thill afurushwa kutoka chama cha La République en marche kwa sababu ya "kauli tata" kuhusu PMA
 • Kenya: Mahakama ya Mazingira yazuia mradi tata wa mitambo ya makaa ya mawe (AFP)
Mashariki ya Kati

Jeshi la Syria lazingira ngome za mwisho za kundi la IS

media Wapiganaji wa serikali ya Syria karibu na mkoa wa Deir Ezzor, Septemba 6, 2017 (picha ya zamani). George OURFALIAN / AFP

Jeshi la serikali ya Syria linaendelea kuziteka ngome za kundi la Islamic State. Siku ya alhamisi jeshi la Syria pamoja na washirika wake walifaulu kuzingira mji wa al-Mayadeen, mojawapo ya miji miwili ambayo iko mikononi mwa kundi la Islamic Sate katika mkoa wa mashariki wa Deir Ezzor.

Jeshi la Syria na washirika wake,wakisaidiwa na jeshi la anga la Urusi, siku ya alhamisi waliweza kudhibiti barabara inayounganisha mji wa al-Mayadeen na mji wa Bou Kamal, kilomita 85 zaidi kusini mwa Syria, kwenye mpaka na Iraq. Hii ni miji miwili ya mwisho ambayo bado inashikiliwa na kundi la Islamic Sate nchini Syria.

Mji wa al-Mayadeen, kutoka kilomita 45 kusini mwa Deir Ezzor, kwa sasa umezingirwa na askari wa serikali, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) na vyanzo vilivyo karibu na serikali ya Damascus.

Al-Mayadeen ni mojawapo ya ngome muhimu zaidi ya kundi la Islamic State.

Wakati huo huo majeshi ya Uturuki yanaendelea na operesheni nchini Syria.

Vikosi vya majeshi ya Uturuki vimesonga mbele katika operesheni ya kijeshi nchini Syria kutokomeza wapiganaji wa jimbo la Idlib.

Magari ya Uturuki yameonekana yakisindikizwa na makundi ya wapiganaji wanaoungwa mkono na Al Qaeda katika jimbo la Idlib, huku kundi la Tahrir al-Sham likimili maeneo karibu na kambi ya majeshi ya Kikurdi ambayo yanapigana dhidi ya IS.

Operesheni hiyo iliyonza siku ya jumamosi inajumuisha majeshi ya Uturuki na yale ya Syria.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema hatavumilia vitendo vyovyote vya kigaidi katika eneo lake.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana