Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-USALAMA

Kasri ya Mfalme yashambuluwa Jeddah, Saudi Arabia

Mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki ambaye alikua ndani ya gari ndogo aliendesha shambulio dhidi ya kasri ya Mfalme wa Saudi Arabia katika mji wa Jeddah. Mtu huyo ambaye alikua hatambuliwi na idara za usalama kwa vitendo vya ugaidi aliwaua kwa risasi askari wawili wa kikosi cha ulinzi wa Mfalme na kuwajeruhi wengine watatu.

Mshambuliaji alipigwa risasi na kikosi cha ulinzi cha mfalme (picha).
Mshambuliaji alipigwa risasi na kikosi cha ulinzi cha mfalme (picha). FAYEZ NURELDINE / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji huyo, raia wa Saudi Arabia, mwenye umri wa miaka 28 anayetambuliwa kwa jina la Mansur al-Amri, aliuawa na kikosi cha ulinzi wa Mfalme baada ya shambulio hilo. Bunduki aina ya Kalashnikovs na mabomo yaliyotengenezwa kienyeji vimekamatwa. Sahmbulizi hilo lilifanyika kwenye kituo cha ugazi cha polisi mbele ya mlango wa magharibi wa karsi la Mfalme mjini Jeddah, ambapo familia ya kifalme wanaendesha shughuli zao wakati wa miezi ya majira ya joto.

Mfalme Salman hakuwepo wakati wa shambulio hilo. Kwa sasa yuko ziarani nchini Urusi. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani haijaeleza aliko mwanae wa kiume, Mohamed bin Salman, ambaye ni mrithi mtarajiwa. Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni za vyombo vya habari, Mohamed bin Salman yupo Jeddah.

Mansour al-Amri haijulikani kwa polisi au kuonekana kuwa na uhusiano wowote na makundi yenye msimamo mkali, amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, akihojiwa na kituo cha televisheni cha al-Arabiya. Uchunguzi unaendelea kujua sababu za shambulio hilo, ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.