Pata taarifa kuu
Kurdistan-SIASA

Haider al-Abadi: Kurdistan inatakiwa kutukabidhi viwanja viwili vya ndege

Serikali ya Kikurdi nchini Iraq inayoongozwa na rais Massoud Barzani imeendelea kupata shinikizo zaidi kutoka kwa majirani saa 48 baada ya wananchi wa eneo hilo kupiga kura ya kutaka kujitawala.

Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi ametoa makataa kwa serikali ya rais Massoud Barzani kuikabidhi viwanja vyake viwili vya ndege vya kikanda cha Erbil na Suleymaniyeh.
Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi ametoa makataa kwa serikali ya rais Massoud Barzani kuikabidhi viwanja vyake viwili vya ndege vya kikanda cha Erbil na Suleymaniyeh. REUTERS/Ahmed Saad
Matangazo ya kibiashara

Matokeo rasmi ya kura hiyo yalitarajiwa kutolewa siku ya Jumanne usiku, lakini baadae tume iliosimamia ikaahirisha na kuahidi kutoa matokeo hayo leo Jumatano, wakati huu majirani wa eneo la Kurdistan nchini Iraq wakipaza sauti kutounga mkono kwa namna yoyote ile kura hiyo.

Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi ametoa makataa kwa serikali ya rais Massoud Barzani kuikabidhi viwanja vyake viwili vya ndege vya kikanda cha Erbil na Suleymaniyeh, na iwapo haitakuwa hivyo, safari zote za ndege za kimataifa kutoka au kuelekea Kurdistan zitasitishwa kuanzia Ijumaa.

Hapo awali waziri mkuu wa Iraq alieleza kwamba Serikali kuu itaweka mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba", ili kudumisha umoja wa Iraq, baada ya Massoud Barzani kutowa wito kwa serikali kuu ya Baghdad kutofunga milango ya mazungumzo.

Siku ya Jumanne usiku kupitia runinga, rais barazani alitowa wito kwa mara nyingine tena wa mazungumzo na kwamba badala ya vikwazo, ni vema kuketi kwenye mexa ya mazungumzo kwa ajili ya kutengeneza hatma bora kwa wakurdi na Waarabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.