Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Rohani: Iran itaendelea kuimarisha uwezo wa kijeshi na makombora

Rais wa Iran Hassan Rohani amesema kuwa nchi yake inajianda kuimarisha uwezo wake wa kijeshi na kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu licha ya ukosoaji kutoka Marekani na Ufaransa.

rais wa Iran Hassan Rohani ameaopa kuwa nchi yake itaendelea na mpango wake wa nyuklia
rais wa Iran Hassan Rohani ameaopa kuwa nchi yake itaendelea na mpango wake wa nyuklia REUTERS/Stephanie Keith
Matangazo ya kibiashara

Rais Rohani ametoa kauli hiyo wakati wa gwaride la kuadhimisha miaka 37 ya vita kati ya Iraq na Iran, mwaka 1980.

"Mkipenda msipeni, tutaimarisha uwezo wetu wa kijeshi unaohitajika kwa ajili ya kuzuia makosa yasitendeke. Si tu kwamba tutaendeleza makombora yetu lakini pia vikosi vya anga, nchi kavu na baharini. Ili kulinda nchi yetu, hatuomba ruhusa kwa mtu yeyote "rais Rohani amesema katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya serikali.

Iran imeendeleza mpango kabambe wa makomboraya masafa marefu katika miaka ya hivi karibuni, hali ambayo inatia wasiwasi Marekani lakini pia Saudi Arabia, baadhi ya nchi za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ufaransa bila kusau Israel,hasimu wake mkubwa.

Tehran inasema mpango wake wa makombora ya masafa marefu ni kujihami tu. "Mamlaka yetu ya kijeshi ... haikuundwa kwa kushambulia nchi nyingine," Rais Rohani ameongeza.

Katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York, rais wa Marekani Donald Trump alishutumu mpango wa nyuklia wa Iran na mpango wake wa makombora ya masafa marefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.