Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-USALAMA

Jeshi la Syria laendelea na mapigano kuuteka mji wa Raqqa

Wanajeshi wa Syria wanaosaidiwa na vikosi maalum vya Marekani wamekabiliana vikali na kundi la wapiganaji wa kundi la Islamic State na kufanikiwa kuwatimua wanamgambo wakijihadi ambao walikuwa wamebaki katika ngome yao ya Raqqa, maafisa wa jeshi la Syria wamesema.

Mapigano yanaendelea kurindima katika mji wa Raqqa, Syria.
Mapigano yanaendelea kurindima katika mji wa Raqqa, Syria. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati vikosi vya Iraq vilianzisha Alhamisi hii operesheni ya kurejesha kwenye himaya yao mji wa Hawija, magharibi mwa mji wenye utajiri wa mafuta wa Kirkuk, baada ya kuwatimua wapiganaji wa kundi la Islamic State.

Mji wa Hawija ni moja ya maeneo yaliodhibitiwa na kundi la Islamic state mwaka 2014.

Operesheni hii iliyotangazwa na Waziri Mkuu wa Iraq Haïdar al Abadi, inakuja siku nne kabla ya kura ya maoni juu ya uhuru wa Kurdistan nchini Iraq, iliyopangwa kufanyika siku ya Jumatatu kaskazini mwa Iraq, hasa katika mji wa Kirkuk.

Abadi alitoa wito wa kufuta kura hiyo inayotambuliwa na Mahakama Kuu kuwa ni "kinyume na Katiba" ya nchi ya Iraq.

Mji wa Hawija, unapatikana kaskazini mwa Baghdad, na ni mojawapo ya maeneo ya mwisho ambayo bado yanadhibitiwa na wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS). Mapigano mengine ya kujitoa mikononi mwa kundi la IS yanaendelea upande wa mashariki wa mpaka wa Syria katika Bonde la Firate.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.