Pata taarifa kuu
SYRIA-MAUAJI-USALAMA

Watu 42 wauawa katika mashambulizi Raqqa

Watu wasiopungua 42 waliuawa siku ya Jumatatu katika mashambulizi ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani katika jimbo la Raqqa, ngome ya kundi la Islamic State (IS) nchini Syria, ambapo mashambulizi mabaya yameongezeka.

Watu 170 wameuawa katika jimbo la Raqqa tangu siku nane silizopta, kwa mujibu wa OSDH.
Watu 170 wameuawa katika jimbo la Raqqa tangu siku nane silizopta, kwa mujibu wa OSDH. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Wanawake 12 na watoto 19 ni miongoni mwa waathirika wa mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa katika maeneo kadhaa kaskazini mwa mji wa Raqqa, ambapo muungano wa kimataifa unasaidia muungano wa Waarabu wa Kikurdi wanaopambana dhidi ya wanajihadi, kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu nchini Syria (OSDH).

Siku ya Jumapili, watu wasiopungua 27 ikiwa ni pamoja na watoto wengi pia waliuawa katika mashambulizi ya angani ya muungano wa kimataifa katika eneo la makazi katika jimbo la Raqqa, ngome kuu ya kundi al IS nchini Syria, kaskazini mwa nchi hiyo inayokumbwa na vita.

Watu 170 wameuawa katika jimbo la Raqqa tangu siku nane silizopta, kwa mujibu wa OSDH.

Kwa mujibu wa kiongozi wa OSDH, Rami Abdel Rahmane, watu huawa kila siku katika mashambulizi ya angani ya muungano wa kimataifa unaundwa na nchi kadhaa na ambao unasaidia kwa mashambulizi ya angani kundi la wapiganaji la Syria Democratic Forces (SDS), muungano wa Waarabu wa Kikurdi waliojikubalisha kutimua kundi la IS katika mji wa Raqqa. Tangu kuingia katika mji huo mwanzoni mwa mwezi Juni, wapiganaji wa FDS wamewatimua wapiganaji wa IS kwa 60% katika mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.