Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFGHANISTAN-USHIRIKIANO

Trump: Niko tayari kushinda vita Afghanistan

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa mpango wake ulikuwa ni wa kuondoa vikosi vya Marekani, lakini badala yake ameamua wanajeshi hao kubakia ili kuzuia kurudia makosa ambayo yalitokea nchini Iraq.

Rais wa Marekani Donald Trump, wakati akitangaza mkakati mpya kwa Afghanistan Agosti 21, 2017 Fort Myer, Virginia.
Rais wa Marekani Donald Trump, wakati akitangaza mkakati mpya kwa Afghanistan Agosti 21, 2017 Fort Myer, Virginia. REUTERS/Joshua Roberts
Matangazo ya kibiashara

Amesema pia kuwa anaongeza idadi ya wanajeshi watakao pelekwa nchini Afghanstan.

“Kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini Afghanistan kutawapa nafasi magaidi kujidhatiti vilivyo, ” amesema Bw Trump.

Bw Trump amesisitiza kuwa kitendo cha Marekani kujiondoa kwa haraka nchini Afghanistan, kitatatoa nafasi kwa ugaidi kujiimarisha zaidi kama ilivyotokea Iraq.

Rais Donald Trump, kupitia Televishen, amesema akisisitiza kuwa kipaumbele cha Marekani ni kutokomeza mtandao wa ugaidi na kutekeleza masuala yenye maslahi katika usalama wa taifa la Afghanistan.

Licha ya kauli hiyo, Bw Trump hakuzungumzia muda wa mwisho wa ushiriki wa Marekani nchini Afghastan na idadi kamili ya ongezeko la wanajeshi.

Wakati huo huo rais Donald Trump amilaumu Pakistan kuwahifadhi magaidi, huku akiitaka nchi hiyo kuachana na mpango huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.