Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Watu 24 Kabul waangamia katika shambulizi la Bomu

Shambulizi la bomu lililotokea katika mji mkuu wa Afghanidstan, Kabul, mapema Jumatatu hii asubuhi lmesababisha vifo vya watu 24 na wengine wengi kujeruhiwa.

Mji wa kabul unaendelea kukumbwa na mashambulizi.
Mji wa kabul unaendelea kukumbwa na mashambulizi. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Lengo la shambulizi hilo halikutajwa mara moja na hakuna mtu aliyedai kuhusika.

Shambulizi hilo litokea karibu na nyumba na afisa wa cheo cha juu serikalini, Mohammad Mohaqiq.

Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Afghanistan, watu 42 pia walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua katika eneo lenye washia wengi magharibi mwa mji.

Mji wa Kabul umekumbwa na mfululizo wa mashambulizi likiwemo lile lililowaua watu 90 wakati lori lililipuka mwezi Mei.

Itakumbukwa kwamba zaidi ya watu 30 waliuawa wakati wa uvamizi wa hospitali ya Sardar Daud mjini Kabul mapema mwezi Mei mwaka 2017

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.