Pata taarifa kuu
JORDAN-ISAEL-USHIRINIANO-USALAMA

Risasi zasikika kwenye ubalozi wa Israel nchini Jordan

Ufyatuaji risasi uliokea kwenye ubalozi wa Israel nchini Jordan umesababisha vifo vya raia wawili wa Jordan na raia mmoja wa Israel amejeruhiwa.

Ufyatuaji huo ulitokea katika jengo moja linalotumiwa na ubalozi wa Israel mjini Amman, Mji mkuuwa Jordan.
Ufyatuaji huo ulitokea katika jengo moja linalotumiwa na ubalozi wa Israel mjini Amman, Mji mkuuwa Jordan. ©Gary Jones/wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Polisi iimezingira ubalozi wa Israel katika mji wa Amman na Israel imechukua uamuzi wa kumewahamisha wafanyakazi. Ubalozi huo wenye ulinzi mkali uko mtaa wa Rabiyeh ambalo ambao ni wa kifahari mjini Amman

Ufyatuaji huo ulitokea katika jengo moja linalotumiwa na ubalozi wa Israel.

Inaarifiwa kuwa watu hao walikuwa wakifanya kazi na kampuni moja ya zamani na waliingia ndani ya ubalozi wa Israel kabla ya ufyatuaji risasi kuanza, kwa mujibu wa polisi.

Israel haijazungumzia kisa hicho. Ripoti chache zimetolewa kuhusu kile kilisababisha kutokea kwa kisa hicho.

Itakumbukwa kwamba siku ya Ijumaa umati wa watu uliingia mitaani mjini Amman kupinga hatua ya Israeal ya kuweka vifaa vya kutambua chuma katika aneo takatifu kwa waislamu na wakiristo mashariki mwa Jerusalem.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.