Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA

Nchi za Kiarabu zaionya Israel kuhusu maeneo takatifu

Muungano wa nchi za kiarabu unasema Israeli inacheza na moto kwa kuweka masharti mapya ya kiusalama katika maeneo ya kuabudu mjini Jerusalem.

Baadhi ya Waislamu wakiwa wamepiga foleni wakikaguliwa kabla ya kuingia msikitini
Baadhi ya Waislamu wakiwa wamepiga foleni wakikaguliwa kabla ya kuingia msikitini REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa muungano huo Ahmed Abul Gheit, amesema  mji wa Jerusalem na maeneo takatifu ni sehemu nyeti sana na mataifa hayo ya kiarabu hayatakubali masharti hayo.

Serikali ya Israel imeweka mitambo ya kuwakagua Waislamu wanaokwenda katika msikiti mkubwa mjini Jerusalem, baada ya kuuawa kwa maafisa wake wawili wa polisi mwezi uliopita waliopigwa risasi.

Hatua hii imesababisha Palestina kusitisha mawasiliano ya karibu na Israeli.

Israeli ambayo imekuwa ikisema ilichukua hatua hii kwa sababu za kiusalama, imesema iko tayari kuzungumzia hatua hii na hata kulegeza masharti haya ya kiusalama.

Wiki hii Waislamu walisusia kuingia katika Msikiti wa Al aqsa kuendelea na ibada zao na kulazimika kuendelea na ibada zao nje ya Msikiti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.