Pata taarifa kuu
IRAQ-ISIS

Amnesty International, yataka kuchunguzwa kwa mauaji ya raia mjini Mosul

Shirika la kimataifa la Kutetea haki za Binadamu la Amnesty International, limetaka kuundwa kwa Tume maalumu kuchunguza makosa ya uhalifu dhidi ya raia yaliyotekelezwa kwenye mji wa Mosul nchini Iraq na pande zote mbili wakati wa vita ya kuukomboa mji huo.

Jeshi la Iraq lasherehekea kuuteka miji wa Mosul
Jeshi la Iraq lasherehekea kuuteka miji wa Mosul © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa Shirika hilo kwa nchi za Mashariki ya kati, Lynn Maalouf amesema kuwa vitendo vya kutisha vilivyoshuhudiwa na wananchi vikitekelezwa na pande zote mbili havipaswi kuachwa bila kuchukuliwa hatua.

Lynn Maalouf amesema kuwa ni lazima tume ya uchunguzi iundwe haraka na kupewa jukumu la kutathmini athari zilizotokana na vita hiyo pamoja na makosa ya uhalifu wa kivita yaliyotekelezwa na pande zote mbili.

Katika hatua nyingine waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi ametangaza kumalizika kwa vita dhidi ya kundi la Islamic State kwenye mji wa Mosul, mji ambao ulichukuliwa na wanajihadi hao miaka mitatu iliyopita.

Waziri Mkuu al-Abadi amesema ushindi ambao vikosi vyake imeupata ni ishara tosha kuwa kundi la Islamic State limedhibitiwa na linaelekea kuanguka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.