Pata taarifa kuu
QATARI=SAUDIA ARABIA-USHIRIKIANO

Qatar yatakiwa kutekeleza masharti ya nchi za kiarabu

Saudi Arabia na washirika wake wa tatu wa kiarabu wametoa muda wa saa 48 kwa Qatar kutekeleza masharti iliyopewa. Nchi hizi nne za kiarabu zimetishia kuiwekea vikwazo Qatar kama haitakubali kutimiza masharti hayo baada ya muda wa saa 48.

Qatar yatakiwa kutekeleza masharti ya nchi za kiarabu kabla ya saa 48 kumalizika.
Qatar yatakiwa kutekeleza masharti ya nchi za kiarabu kabla ya saa 48 kumalizika. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Qatar imesema itajibu kupitia barua iliyowasilishwa kwa Kuwait Jumatatu hii Julai 3.

Qatari imekua ikilaumiwa na majirani zake kwamba inahifadhi itikadi za kali za kigaidi, lakini imesema ni madai yasio kuwa na msingi.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, anatazamiwa kusafiri kwnda Kuwait baadae leo, kuwasilisha barua hiyo iliyotumwa kutoka kwa kiongozi wa Qatar kuenda kwa kiongozi wa kuwait ambaye ni mpatanishi mkuu wa mzozo kati ya mataifa hayo ya kiarabu.

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani, alisema kuwa nchi yake ililikataa masharti hayo lakini iko tayari kwa mazungumzo.

Tarehe ya mwisho ya kuitaka Qatar kukubali masharti 13, ikiwemo ya kukifunga kituo cha Al Jazeera ilimalizika jana Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.