Pata taarifa kuu
ISRAEL

Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ehud Olmert aachiwa huru

Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ehud Olmert ameachiwa huru kutoka jela, baada ya kusamehewa kwa kosa la ufisadi.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert REUTERS/Debbie Hill
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuachiwa huru, Olmert hakusema lolote kwa wanahabari waliomsubiri nje ya jela ya Maasiyahu katikati ya nchi hiyo.

Olmert mwenye umri wa miaka 71, aliongoza nchi hiyo kati ya mwaka 2006 na 2009.

Baada ya kubainika kuhusika na ufisiadi, Olmert alihukumiwa jela miezi 27 mwezi Februari mwaka 2016.

Waziri Mkuu huyo wa zamani alijiuzulu mwezi Septemba mwaka 2008 baada ya idara ya Polisi kutoa ripoti na kutaka afunguliwe mashtaka ya ufisadi.

Hatua ya kuachiliwa kwake imekuja baada ya hivi karibuni kukimbizwa hospitalini, baada ya kuanza kushuhudia maumivu ya kifua.

Bodi inayosimamia msamaha wa wafungwa imesema kuwa inaamini kuwa Olmert amejutia makosa aliyofanya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.