Pata taarifa kuu
ISRAEL-OLMERT-HAKI

Aliekua Waziri mkuu wa Israel aachiwa huru kwa dhamana

Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Ehud Olmert, ambaye anatumikia kifungo cha miaka miwili na miezi mitatu jela kwa kosa la rushwa, amefanikiwa Alhamisi hii kuachiwa huru kwa masharti, mmoja wa mawakili wake amesema.

Aliekua waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert, baada ya kutangazwa hukumu dhidi yake ya kutumikia kifungo cha miezi 18 jela.
Aliekua waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert, baada ya kutangazwa hukumu dhidi yake ya kutumikia kifungo cha miezi 18 jela. REUTERS/Debbie Hill
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni kituo cha radio ya taifa nchini Israel, ilitangaza kwamba Ehud Olmert anaweza kuachiwa huru siku ya Jumapili, kifungo chake kilipunguzwa, utaratibu unaotumiwa nchini Israel kwa wafungwa ambao hawajafanya uhalifu mkubwa.

Kuachiliwa kwake kunaweza kuchelewa ikiwa waendesha mashitaka wataamua kukata rufaa, Shani Eluz, mmoja wa washauri wa waziri mkuu wa zamani wa Israel amewaambia waandishi wa habari.

Ehud Olmert alipatikana na hatia mwaka 2014 ya kukubali kupokea rushwa kutoka kampuni kadhaa wakati ambapo alikua Meya wa Mji wa Jerusalem kabla ya kuwa waziri mkuu mwaka 2006 hadi 2009 na kiongozi wa chama cha kisiasa cha mrengo wa kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.