Pata taarifa kuu
QATAR-DIPLOMASIA-USALAMA

Qatar yasema haitatikiswa licha ya kutengwa kwa madai ya ugaidi

Qatar inasema itaendelea kufanikiwa, kuwepo na kuwa imara licha ya kutengwa kidiplomasia na mataifa sita ya kiarabu kwa madai kuwa inafadhili na kuwaunga mkono magaidi.

Waziri wa Mambo ya nje wa Qatar  Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani
Waziri wa Mambo ya nje wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani almanar.com.lb
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa, Doha inaheshimu sheria na mikataba ya za Kimataifa.

Aidha, amesema kama taifa linaloongoza katika usafirashaji wa gesi nje ya nchi, itaendelea kusafirisha bidhaa hiyo muhimu kwa nchi ya Falme za Kiarabu.

Mataifa yaliyositisha uhusiano wake wa kidiplomasia ni pamoja na Saudi Arabia, Bahrain, Falme za Kiarabu, Yemen, Libya na Misri.

Qatar imekanusha madai dhidi yake na kusema hakuna ushahidi wa kuthibitisha hilo.

Marekani imesema iko tayari kuwaleta pamoja viongozi wa mataifa ya ghuba ili kujadili mzozo huu.

Hata hivyo, Qatar inasema hakuna anayewezesha kushawishi sera yake ya mambo ya nje.

Iran, Kuwait na Uturuki zimependekeza kuwepo kwa mazungumzo ili kumaliza mzozo huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.