Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 13/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Saudia yakaribisha mkataba wa amani nchini Yemen na kutangaza kusaidia kupatikana kwa suluhu ya kisiasa
Mashariki ya Kati

Trump kukutana na Mahmoud Abbas Jumanne hii

media Donald Trump mbele ya ukuta wa Ukuta wa Maombolezo mjini Jerusalem , Mei 22, 2017. REUTERS/Jonathan Ernst

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kukutana na kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, Jumanne hii ni siku ya pili ya ziara yake katika eneo la Mashariki ya Kati, baada ya kukutana siku ya Jumatatu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pamoja na rais wa nchi hiyo.

Ziara hiyo ya siku mbili nchini Israel na katika utawala wa Palestina ni sehemu ya ziara ya kwanza ya kigeni ya bwana Trump.

Rais Trump anajitambua kama mpatanishi mkuu wa kutatua masuala ambayo yamewashinda watu wengi.

Suala kuu ni kubuniwa kwa taifa huru la palestina kando ya Israel.

Eneo la ukingo wa Magharibi pamoja na mashariki mwa mji wa Jerusalem limekaliwa na Israeli kwa miaka 50.

Baadhi ya watu wenye ushawishi ndani ya serikali ya Israel wanaamini kuwa ardhi hiyo ni ya Waisraeli waliyopewa na Mwenye Enzi Mungu.

Siku ya Jumatatu Trump alisema kuwa kuna ushirikiano mkubwa kati ya Marekani na Israel, huku akionya juu ya kuwepo kwa tishio la Iran kwa usalama wa dunia

Itafahamika kwamba Israel na Palestina hawajafanya mazungumzo ya moja kwa moja kwa zaidi ya miaka mitatu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana