Pata taarifa kuu
SYRIA-MAZUNGUMZO

Mazungumzo mapya ya amani kurejelewa Syria

Mazungumzo kati ya serikali ya Damascus na upinzani yanaanza Jumanne hii mjini Geneva. Lakini hakuna matumaini yoyote ya kupata matokeo mara moja. Mazungumzo ya mjini Geneva chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa yanakabiliwa na mazungmzo sambamba yanayoendeshwa na Urusi, Iran na Uturuki katika mji wa Astana.

Staffan de Mistura, Januari 12, 2017 Geneva.
Staffan de Mistura, Januari 12, 2017 Geneva. REUTERS/Pierre Albouy/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura, anaonekana kwa sasa mtu pekee ambaye atafanikisha mazungumzo haya.

Staffan de Mistura anaendeleza mfululizo wa mazungumzo baina ya Wasyria na amekua akirejelea hotuba ile ile: "Kuna matokeo yenye matumaini."

Hata hivyo tangu mwaka jana, Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria amekutana mara nne na utawala pamoja na upinzani bila kupata matokeo yoyote.

Lakini katika mkutano wa mwisho, washiriki walikubaliana kujadili mada nne:

- Ni nani atakaetawala Syria ya kesho?
- Mageuzi ya Katiba
- Maandalizi ya uchaguzi huru
- Mapambano dhidi ya "ugaidi"

Kama mazungumzo ya moja kwa moja yatafanikiwa katika kikao hiki kipya cha mazungumzo, itakuwa ni ushindi. Vinginevyo, Staffan de Mistura, mwenye umri wa miaka 70, itabidi ashawishi serikali na upinzani kufikia makubaliano ya kudumu.

Tayari inajulikana, mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria anataka kushughulikia masuala makubwa. Lengo lake ni kukomesha mapigano kwenye uwanja wa vita na wakati huo huo kuwenda na makubaliano ya kusitisha mapigano kwa kupitia mazungumzo kuhusu mustakabali wa kisiasa wa Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.