Pata taarifa kuu
UFARANSA-SYRIA-USALAMA

Ufaransa: Syria ilitumia gesi ya Sarin katika mji wa Khan Cheikhoun

Ufaransa inasem ahivi karibuni itatoa "ushahidi" kwamba utawala wa Bashar Assad ulihusika kwa mashambulizi ya kemikali ambayo yalisababisha vifo vya watu 87 wakiwemo watoto 31 Aprili 4 nchini Syria. Waziri wa mambo ya Nje wa Ufaransa ameyasema hayo siku ya Jumatano, Aprili 19.

Khan Cheikhoun: mji uliyoshambuliwa mara mbili ambapo mara ya kwanza ulishambuliwa kwa gesi yenye sumu, Jumanne, Aprili 4, 2017.
Khan Cheikhoun: mji uliyoshambuliwa mara mbili ambapo mara ya kwanza ulishambuliwa kwa gesi yenye sumu, Jumanne, Aprili 4, 2017. REUTERS/Ammar Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Syria imekanusha madai hayo, miaka mitatu baada ya kutokomeza silaha zake za nyuklia.

Shirika la linalopiga marufuku silaha za maangamizi (OPCW) hatimaye limeelezea kuwa gesi aina ya sarin au gesi yenye sumu inayofanana hiyo iliua watu 87 katika mji wa Syria wa Khan Cheikhoun.

Katika hatua hii, OPCW haijaweka wazi kundi lililohusika. Hata hivyo nchi nyingi, zinaishtumu serikali ya Bashar al-Assad kuhusika na kitendo hicho. Marekani hata hivyo iliemdesha mashambulizi ya kulipiza kisasi katika kambi moja ya kijeshi ya Syria bombed msingi Syria katika kulipiza kisasi.

Ufaransa pia ainaituhumu Damascus na siku ya Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje Jean-Marc Ayrault aliahidi kutoa ushahidi katika siku zijazo.

Wakati huo huo ikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, Jean-Marc Ayrault alikosoa utaratibu "usiofurahisha" unaotumiwa na baadhi ya wagombea kuhusiana na Assad na mshirika wake Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.