Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Mahakama yampa ahueni waziri mkuu wa Pakistan

Mahakama ya juu nchini Pakistan imetoa uamuzi kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu tuhuma za rushwa ambazo zingepelekea kuondolewa madarakani kwa waziri mkuu Nawaz Sharif kwenye nafasi yake.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo kwenye hukumu yake, mahakama hiyo imeagiza kufanyika kwa uchunguzi zaidi kuhusu namna fedha zilivyokuwa zikihamishwa.

Maswali yaliibuka kuhusu biashara za familia ya Sharif ambapo watoto wake wa tatu walihusishwa kwa kuwa na akaunti nje ya nchi kwenye nyaraka zilizovuja mwaka 2015 maarufu kama Panama Papers.

Waziri mkuu Sharif mwenyewe pamoja na familia yake wamekana kufanya makosa yoyote yaliyoashiria vitendo vya rushwa, wakihusisha kesi hii na wapinzani wao kisiasa.
Keso hii ilikuwa gumzo hivi karibuni nchini Pakistan wakati huu ambapo kulikuwa na utabiri kuwa uamuzi wa mahakama ungetoa hatima ya waziri mkuu Sharif.

Zaidi ya polisi elfu 1 na 500 walisambazwa kuzingira mahakama hiyo ya mjini Islamabad, huku waandamanaji waliokuwepo jirani wakitaka waziri mkuu Sharif ajiuzulu nafasi yake.
Hali ya masoko ya hisa nchini Pakistan iliimarika zaidi kutokana na uamuzi huu wa mahakama.

Mahakama ya juu ilikubali mwaka jana kufanyika uchunguzi wa akaunti na utaji alionao waziri mkuu Sharif nje ya nchi baada ya kinara wa upinzani Imran Khan kutishia kuitisha maandamano.

Kiini cha uchunguzi wenyewe kilikuwa ni kuhusu ununuzi wa mali iliyonunuliwa jijini London kwa kutumia akaunti za nje.

Mtoto wa kike wa Nawaz, Maryam anayetajwa kuwa mrithi wa siasa za baba yake na mtoto wake Hasan na Hussein wanahusishwa kwenye tuhuma hizi.

Waziri mkuu Sharif anasema utajiri wake umepatikana kihalali, lakini wakosoaji wake wanadai kampuni zake za nje ya nchi zimekuwa zikitumiwa kukwepa kodi.

Majaji wawili waliunga mkono waziri mkuuj Sharif kuondolewa madarakani lakini majaji wa tatu walikubaliana na kuagiza uchunguzi kufanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.