Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Watoto wengi wauawa katika shambulio la kigaidi la Jumamosi

Nchini Syria, zoezi la kuwahamisha maelfu ya wakazi wa miji ya Foua na Kafraya itaendelea licha shambulizi la kujitoa mhanga la Jumamosi Aprili 15 lililowaua watu wasiopungua 126, ambapo zaidi ya nusu ya waliouawa ni watoto.

Kwa uchache watoto 68 ni miongoni mwa watu 126 waliouawa katika shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya basi lililokua likibeba wakaazi waliokua wakihamishwa.
Kwa uchache watoto 68 ni miongoni mwa watu 126 waliouawa katika shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya basi lililokua likibeba wakaazi waliokua wakihamishwa. REUTERS/Ammar Abdullah TPX IMAGES OF THE DAY
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo imeendelea kuongezeka, hasa wale ambao waliojeruhiwa vikali, na idadi kubwa ya waathirika ni watu kutoka miji ya Foua na Kafraya, wengine ni waasi waliokua wakilinda mabasi ambamo walikuwawemo watu waliokua wakihamishwa pamoja na wafanyakazi wa mashirika ya misaada.

Kwa uchache watoto 68 walikuwa miongoni mwa watu 126 waliouawa katika shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya basi lililokua likibeba wakazi waliokua wakihamishwa kutoka miji inayokaliwa na waasi, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa Jumapili na shirika lisilokua la kiserikali.

Jumapili hii, Aprili 16, miili mingi ilikua bado ikionekana katika eneo la shambulizi, na karibu ya miili hiyo kulikuepo na vifaa kama vile nguo, televisheni au sahani za wahanga hao.

Inaarifiwa kuwa mshambuliaji alitumia gari ndogo la mizigo kwa kutekeleza shambulizi hilo.

Serikali ya Syria inayatuhumu "makundi ya kigaidi" kuwa ndio yalitekeleza shambulizi hili. Neno hili hutumiwa na unatwala wa Bashar al-Assad kwa kuwataja waasi na wanajihadi. Lakini kundi la waasi lenye ushawishi mkubwa la Ahrar al-Sham limekanusha kuhusika kwa wapiganaji katika shambulio hilo.

Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema kuhadhabishwa na kushambulio hilo, lililoshtumiwa pia na nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.