Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFGHANISTAN-USALAMA

Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa nchini Marekani azuru Afghanistan

Mkuu wa Baraza la Usalama wa taifa nchini Marekani, Jenerali H. R. McMaster, amekutana kwa mazungumzo Jumapili hii April 16 na Rais Ashraf Ghani kuhusu masuala ya usalama na kukabiliana na ugaidi.

Jeneral H. R. McMaster, mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa nchini Marekani Marekani.
Jeneral H. R. McMaster, mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa nchini Marekani Marekani. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inakuja siku nne baada ya Marekani kuendesha hambulio la bomu aina ya GBU-43 mashariki mwa Afghanistan na kuharibu mapango na vichuguu vinavyotumiwa na kundi la Islamic State kama maficho na njia wanazotumia kwa kuendesha mashambulizi mbalimbali nchini humo. Mamlaka ya Afghanistan wametoa ripoti ya kwanza ya operesheni hiyo. Zaidi ya wapiganaji 90 waliuawa kwa mujibu wa serikali, huku ikieleza operesheni hiyo imepata mafanikio makubwa.

Tumejitahidi kufaanikisha katika operesheni tuliofanya hivi karibuni, amesema msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan, akibaini kwamba maeneo ya maficho ya kundi la Islamic State katika wilaya ya Achin yaliharibiwa na mama wa mabomu yote. Bomu kubwa, lenye kilo 9 ya vilipuzi, lililipuka kabla ya kudondoshwa ardhini kwenye eneo la mita 150. Bomu hili lilikua ni silaha pekee yenye uwezo wa kuharibu maeneo ya maficho ya ardhini ya magaidi, ambalo linachimba hadi mita 40 ya kina.

Bomu kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa na Marekani na ambalo halitumii nyuklia liliangushwa kwenye milima ya Afghanistan na kuwaua mamia ya wapiganaji wa kundi la Islamic State ambao walikuwa wakijificha kwenye mahandaki.

Bomu hili aina ya GBU-43/B Massive Ordnance Air Blast lilitarajiwa kumaliza kabisa uwezo wa kundi la Islamic State nchini Afghanistan na kutuma onyo kwa kundi la Taliban ambalo linajiandaa na mashambulizi yake ya mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.