Pata taarifa kuu
SYRIA-MLIPUKO

Syria: Mlipuko mkubwa waua raia waliokuwa wanaokolewa Aleppo

Mlipuko mkubwa umesababisha vifo vya mamia ya watu katika shambulio lililotekelezwa jirani na mabasi yaliyokuwa yamewabeba raia waliokuwa wakihamishwa kutoka kwenye miji miwili inayokabiliwa na mashambulizi ya Serikali.

Moshi mkubwa ukiwa umetanda punde tu baada ya mlipuko uliolenga msafara wa mabasi ya raia waliokuwa wanaokolewa mjini Aleppo, Syria.
Moshi mkubwa ukiwa umetanda punde tu baada ya mlipuko uliolenga msafara wa mabasi ya raia waliokuwa wanaokolewa mjini Aleppo, Syria. Social Media Website via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko kwenye mji wa Rashidin, magharibi mwa Aleppo, ulilenga wakazi ambao walikuwa wakiokolewa kutoka kwenye miji ya waasi inayoshambuliwa na Serikali hasa kwenye maeneo ya Fouaa na Kefraya kwenye jimbo la Idlib chini ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya waasi na Serikali ya Syria.

Taarifa iliyorushwa na kituo cha televisheni ya Serikali imesema kuwa watu 39 wameuawa kwenye shambulio hilo. Huku shirika moja la haki za binadamu lenyewe likisema waliokufa ni zaidi ya 43.

Wakati huu kukiwa hakuna taarifa rasmi kuhusu sababu za mlipuko huo, televisheni ya taifa imesema ni shambulio la kujitoa muhanga lililotekelezwa kwa kutumia gari dogo lenye kubeba dawa za msaada lililokuwa likiingia kwenye mjik huo.

Taarifa za makundi mengine ya kibinadamu zinasema mlipuko ulitoka kwenye gari dogo lililokuwa jirani.

Mashuhuda wa tukio lenyewe wanasema mamia ya miili ya watu ilionekana kurushwa kwenye ardhi toka kwenye mabasi na magari ya kubebea wagonjwa yalijaa majeruhi wa shambulio hili.

Picha zilizochapishwa kwenye vyombo vya Serikali zinaonesha kile kinachoelezwa kuwa ni athari za baada ya shambulio, ambapo miili inaonekana imechomeka na moshi mweusi ukiwa umetanda.

Mabasi kadhaa yaliwaka moto huku mengine yakiharibiwa vibaya kutokana na athari za mlipuko.

Mwandishi wa kituo cha habari cha Aljazeera Hoda Abdel-Hamid ambaye amekuwepo kwenye tukio, amesema inaonekana mlipuko ulitokea mbele ya msafara wa mabasi ya awali ambayo yalikuwa kama 70.

Shambulio limetokea wakatik maelfu ya raia wanaookolewa kutoka kwenye miji inayoshambuliwa na Serikali wakisubiri kuendelea na safari yao kwenda kwenye miji inayokaliwa na vikosi vya Serikali kwenye mji wa Aleppo, jimbo la Latakia na jiji kuu Damascus.

Zaidi ya watu elfu 5 ambao wameishi kwenye miji hiyo yenye mapigano kwa muda wa miaka miwili wameondoka kwenye miji hiyo, sambamba na wengine elfu 2 waliookolewa kutoka kwenye miji inayokaliwa na waasi ya Madaya na Zabadani sikuj ya Ijumaa.

Zoezi la kuwahamisha raia liliratibiwa na utawala wa Iran unaoiunga mkono Serikali na Serikali ya Qatar inayowaunga mkono waasi na itashuhudia watu zaidi ya elfu 30 wakihamishwa kwa awamu mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.