Israel yaendesha mashambulizi katika Ukanda wa Gaza
Ndege za kijeshi za Israel ziliendesha mashambulizi Jumatatu hii katika Ukanda wa Gaza na kusababisha watu wanne kujeruhiwa. serijkali ya Israel inasema imechukua uamuzi wa kuendesha mashambulizi hayo baada ya kitendo cha watu wasiojulikana kurusha roketi kusini mwa Israel.
Imechapishwa:
Jeshi la Israel linasema lililenga ngome tano za kundi la Hamas, kundi la Kiislamu linalodhibiti ardhi ya Palestina kwa karibu miaka kumi.
Kwa mujibu wa serikali ya Israel, roketi ilianguka katika eneo lisilokua na watu na haikusababisha hasara yoyote.
Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na kitendo hicho, lakini serikali ya Israel inalinyooshea kidole cha lawama kundi la Hamas linahusika kwqa kuzorotesha usalama katika eneo linalodhibiti tangu Juni 2007.
Kundi hili la Kiislamu lilisitisha mapigano kimyakimya tangu mashambulizi ya Israel mwaka2014, lakini kuna baadhi ya wanajihadi kutoka kundi hilo ambao mara kwa mara wamekua wakirusha roket nchini Israel.
Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman amesema Israel "haikua na nia yoyote ya kushiriki katika operesheni yoyote ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza, lakini haitovumilia kitendo cha kurusha roketi katika baadhi ya maeneo yake".
Fawzi Barhoum, Msemaji wa Hamas, amesema Israel itahusika na kuongezeka ka machafuko kama itaendelea kulenga "ngome za Hamas".