Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA-USALAMA

Marekani yatuma magari ya kijeshi kusaidia waasi wa FDS nchini Syria

Muungano wa kimataifa unaongozwa na Marekani dhidi ya kundi la Islamic State umetoa msaada wa magari ya kijeshi kwa waasi wa Syria ambao ni washirika wake. wanaojiandaa katika vita vya kuuteka mji wa Rakka, mji mkuu" wa kundi la IS.

Wapiganaji wa kundi la wasi wa Syria la FDS katika kijiji cha Haj Hussein, kusini ya mji wa Manbij Mei 31, 2016.
Wapiganaji wa kundi la wasi wa Syria la FDS katika kijiji cha Haj Hussein, kusini ya mji wa Manbij Mei 31, 2016. REUTERS/Rodi Said
Matangazo ya kibiashara

Kundi hili la waasi la FDS, lenye wapiganaji wengi kutoka jamii ya Wakurdi wa kundi la YPG, linapamana dhidi ya IS kaskazini mwa Syria, ikiwa ni pamoja na kuuteka mji wa Rakka.

Msemaji wa kundi la waasi la FDS, Talal Silo, amesema kuwa utoaji wa magari ya kivita ni ishara ya ushindi na kupongeza utawala mpya wa Marekani. Katika kampeni zake, Donald Trump alisema kuwa kulitokomeza kundi la IS ni moja ya vipaumbele vyake.

"Tunaona dalili za msaada kamili wa utawala mpya wa Marekani kwa majeshi yetu, zaidi kuliko kabla, " amesema Talal Shilo. "Hapo awali, tulikua hatupati aina hii ya msaada, tulikua tukipewa tu silaha ndogo ndogo za kivita, " Bw Shilo ameongeza.

Msemaji wa Pentagon amesema kuwa magari ya kivita yalitolewa kama saada kwa muungano wa Kiarabu nchini Syria, ikiwa ni pamoja na kundi la FDS. Huu ni msaada wetu tunatoa kwa kusaidi kundi hili kwa minajili ya kuuteka mji wa Rakka, unaokabiliwa na kitisho cha milipuko ya mabomu ya yanayotengenezwa kienyeji na kutumiwa na kundi la IS, msemaji wa Pentagon Meja Adrian J.T. amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.