Pata taarifa kuu
SYRIA-MAZUNGUMZO

Mkutano wa Astana: Urusi, Uturuki na Iran zakubaliana kusitishwa kwa vita Syria

Wadhamini watatu wa mazungumzo ya amani nchini Syria,Urusi, Uturuki na Iran wamekubaliana kuweka utaratibu wa utekelezaji na ufuatiliaji wa mkataba wa usitishwaji vita ulioafikiwa nchini Syria tangu mwezi Desemba 30. Nakala ya mwisho haikusainiwa na wajumbe wa makundi ya waasi wala wale wa Bashar Al Assad.

Wajumbe katika mkutano wa mjini Astana, Januari 23, 2017.
Wajumbe katika mkutano wa mjini Astana, Januari 23, 2017. REUTERS/Mukhtar Kholdorbekov
Matangazo ya kibiashara

Mkutano katika mji wa Astana umemalizika kwa tamko la pande tatu Urusi, Uturuki, Iran, nchi tatu zilizofadhiliwa mazungumzo hayo. Hata hivyo, serikali ya Syria wala makundi ya waasi nchini humo hawakusaini nakala ya mwiho ya mazungumzo hayo, na hawakuwa wamewakilishwa katika ukumbu kulikofanyika mazungumzo hayo wakati ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Kazakhstan aliposona nakala hiyo.

Nchi hizi tatu zilitangaza kuwekwa kwa utaratibu utakaosimamia mkataba wa usitishwaji mapigano. Kwa mengine yanayosalia, nchi hizi zinasisitiza juu ya mgawanyo wa makundi ya waasi na makundi ya kigaidi, na zinaunga mkono majadiliano ya kisiasa ambayo yatafanyika tarehe 8 Februari mjini Geneva.

Mbali na kuwekwa kwa utaratibu huu wa nchi tatu ikiwa ni pamoja na Iran, mkutano wa Astana ulitathimini kuhusu baadhi ya maswala. Iran imehusishwa, na jambo hili ni jipya ikilinganishwa na mkataba wa usitishwaji mapigano wa tarehe 29 Desemba.

Lakini upande wa waasi wamekata tamaa. Katika mkutano huo hawakuzungumzia kuhusu wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran.

Awali waasi walitishia kuanzisha vita iwapo mazungumzo yatashindwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.