Pata taarifa kuu
SYRIA-MAZUNGUMZO

Waasi wa Syria waapa kuendeleza vita kama mazungumzo ya Astana yatashindwa

Mazungumzo ya amani kuhusu mzozo wa Syria yameanza kwa mashaka jijini Astana, nchini Kazakistan Jumatatu wiki hii. Makundi ya waasi na serikali wanashiriki mazungumzo haya, lakini waaasi wametishia kuenelea na vita kama mazungumzo yatashindwa.

Mazungumzo ya amani kuhusu Syria yafadhiliwa na Urusi, Uturuki na Iran katika mji wa Astana, nchini Kazakhstan, Januari 23, 2017.
Mazungumzo ya amani kuhusu Syria yafadhiliwa na Urusi, Uturuki na Iran katika mji wa Astana, nchini Kazakhstan, Januari 23, 2017. REUTERS/Mukhtar Kholdorbekov
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya amani kuhusu mzozo wa Syria yameanza kwa mashaka jijini Astana nchini Kazakistan.

Imekubaliwa kuwa wawakilishi wa waasi na serikali hawatakutana ana kwa ana katika mazungumzo hayo ambayo waasi wanasema yatafanikiwa tu ikiwa vita vitasitishwa kabisa katika ngome zao kama anavyoleza Yahya al-aridi msemaji wa waasi katika mazungumzo haya.

Hata hivyo, serikali ya Syria kupitia Balozi wake katika Umoja wa Mataifa Jafar Bashaar amesema kuwa waasi wanaleta vikwazo na hawakuelewa mantiki ya mkataba wa kusitishwa kwa vita nchini Syria.

Akifungua mkutano huo, Waziri Mkuu wa Kazakistan Kairat Abdrakhmanov amesema kuwa ana imani kuwa mazungumzo haya yataleta amani ya kudumu nchini Syria ili kumaliza vita vya miaka sita.

Mataifa ya Urusi, Iran na uturuki ndio waandalizi wa mazungumzo haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.