Pata taarifa kuu
UKRAINE-ISRAEL-USHIRIKIANO

Azimio juu ya makazi ya Wayahudi Ukingo wa Magharibi mvutano kati ya Ukraine na Israel

Israel ilihirisha ziara ya Waziri Mkuu wa Ukraine Volodymyr Groisman Jumamosi mjini Jerusalem, kwa sababu ya Ukraine kuunga mkono azimio la hivi karibuni la Umoja wa Mataifa dhidi makazi ya Wayahudi katika maeneo yanayoshikiliwa ya Palestina. Tangu wakati huo, uhusiano si mzuri kati ya nchi hizi mbili, ambazo ziliwaita mabalozi kutoka nchi hizo ili waweze kujieleza.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Ukraine Volodymyr Groisman, Israel imefutwa.
Ziara ya Waziri Mkuu wa Ukraine Volodymyr Groisman, Israel imefutwa. AFP/John MacDougall
Matangazo ya kibiashara

Ukraine imekua ikionyesha msimamo wake kwa tahadhari kuhusu mgogoro wa Israel na Palestina. Lakini wakati huu imeamua kuonyesha wazi kuwa haiungi mkono ujenzi wa makazi katika maeneo ya Palestina, jambo ambalo limeikasirikisha Israel.

Uamuzi wa kufutwa kwa ziara ya Volodymyr Groisman nchini Israel umechukiwa kwa shingo upande na serikali ya Kiev. Kwa sababu Waziri Mkuu wa Ukraine ni kiongozi pekee wa Ulaya anayeonyesha msimamo wake wa Kiyahudi. Hata hivyo bado ana ndugu nchini Israeli, na serikali ya sasa nchini Ukraine ilikua inapanga kufanya ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi na Israel.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Wizara ya Mambo ya Nje yaUkraine ilitoa taarifa ya wazi ikikosoa mwenendo wa Israeli kufuatia kura ya Umoja wa Mataifa.
Matokeo yake, Jumapili na Jumatatu nchi hizo mbili ziliwataka mabalozi kutoka nchi hizo kujieleza.

Kwa kueleza msimamo wake juu ya azimio la Umoja wa Mataifa, serikali ya Ukraine imesema kuwa hata yenyewe ni mwathirika wa uvamizi na kushikiliwa na Urusi, katika eneo la Crimea na mashariki mwa Ukraine. Kwa hiyo Kiev inataka sheria za kimataifa ziheshimiwe kila mahali, nchini Ukraine sawa na Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.