Pata taarifa kuu
PAKISTAN-AJALI

Hakuna aliyenusurika katika ajali ya ndege ya PIA

Ndege ya shirika la ndege la Pakistan International Airlines ilianguka wakati ilipokua ikifanya safari ya ndani kati ya mji wa Chitral, katika eneo la milima kaskazini mwa nchi na mji mkuu Islamabad. Ndege hiyo ilitoweka kwenye rada muda mfupi baada ya kupaa angani Jumatano wiki hii. Ndege hiyo ilianguka kilomita 130 kaskazini mwa mji wa Islamabad, karibu na mji wa Havelian.

Ndege sawa na yenye ilianguka ikijiandaa kuruka mwaka 2015. Ndege za shirika la PIA zilipigwa marufuku na Umoja wa Mataifa kuelekea barani Ulaya mwaka 2007.
Ndege sawa na yenye ilianguka ikijiandaa kuruka mwaka 2015. Ndege za shirika la PIA zilipigwa marufuku na Umoja wa Mataifa kuelekea barani Ulaya mwaka 2007. REUTERS/Faisal Mahmood/
Matangazo ya kibiashara

Ndege yenye chapa PK 661, iliyokua ikitokea katika mji wa Chitral, kaskazini mwa nchi, ilikua ikitarajiwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Islamabad siku ya Jumatano jioni. Lakini ndege hiyo ilianguka kilomita arobaini kaskazini mwa mji mkuu. Abiria 42 na wafanyakazi 5 walikuwa ndani ya ndege hiyo aina ya ATR 42 ya shirika la ndege la Pakistan International Airlines. Miongoniu mwao, walikuemo raia watatu wa kigeni na muimbaji maarufu nchini Pakistan, Junaid Jamshed, ambaye alikuwa akisafiri na familia yake. Hakuna aliyenusurika katika ajali hiyo.

Jeshi limetuma haraka vifaa vya uokozi katika eneo la tukio. Picha za awali zilionyesha moto ukiwaka kwenye kilima, ambapo katika moto huo mabaki ya ndege yalikua yakionekana. Hali ya hewa ilikuwa nzuri na tayari vyombo vya habari nchini Pakistan vimebaini kuwa kulikua na tatizo la kiufundi kwenye injini ya kushoto. Lakini serikali, sawa na shirika la ndege la Pakistan International Airlines, wamethibitisha kwamba kwa sasa hawana taarifa sahihi na zenye kuaminika.

Itafahamika kwamba Umoja wa mataifa ilipiga marufuku ndege za shirika hilo la PIA kuelekea barani Ulaya mwaka 2007 kutokana na hali yao ya kiusalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.