Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Watu 58 wauawa katika shambulizi dhidi ya chuo cha polisi mjini Baluchistan

media Chuo cha mafunzo cha polisi katika mji wa Quetta, ambapo shambulizi lilitokea usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne Oktoba 25, 2016, kilomita ishirini kutoka mji mkuu wa Baluchistan. REUTERS/Naseer Ahmed

Kundi la watu wenye silaha wameendesha shambulizi dhidi ya chuo cha polisi, usiku wa kuamkia Jumanne hii Oktoba 25, 2016 kilomita zaidi ya ishirini kutoka katika mji wa Quetta, kusini magharibi mwa Pakistan. Watu wasiopungua 58 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, wengi wao wako katika hali mbaya.

Ilikuwa karibu saa 4:00 (saa za Pakistan) Jumatatu usiku, wakati washambuliaji wenye silaha za kivita waliposhabulia kituo cha mafunzo cha polisi kilomita zaidi ya ishirini kutoka katika mji wa Quetta, katika mkoa wenye usalama mdogo wa Baluchistan.

Shambulio lilianza kwa risasi za hapa na pale, kisha washambuliaji walifanikiwa kupenya na kuingia katika mabweni ambako polisi 700 waliosajiliwa wanalala. Kwa mujibu wa jeshi la Pakistan, watu 200 pekee ndio walikuwepo katika kituo cha mafunzo wakati wa shambulizi hili.

Shambulizi hili lilidumu masaa sita. Askari wengi na polisi walitumwa haraka kukabiliana na kundi hili la washambuliaji.

Hakuna kundi lolote mpaka sasa limedai kuhusika na shambulizi hili. Lakini viongozi wa Pakistan wamesema shambulizi hili limetekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Laskar-e-Jhangvi, lenye mafungamano na kundi la Taliban.

Kituo cha mafunzo cha polisi kinapatikana kilomita sitini na mpaka wa Afghanistan, katika mkoa wa Baluchistan unaojulikana kuwa moja ya ngome za kundi la Taliban.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana