Pata taarifa kuu
SYRIA-HOLLANDE

Hollande atoa wito kwa washirika wa Assad "kufikiria amani"

Rais François Hollande ametoa wito Jumanne hii Septemba 20 kwa jumuiya ya kimataifa kumaliza mgogoro nchini Syria. "Nina neno moja tu la kusema: inatosha", amesema rais wa Ufaransa, huku akiinyooshea kidole serikali ya Syria katika kushindwa kwa mkataba wa usitishwaji wa mapigano uliofikiwa chini ya mwamvuli wa Marekani na Urusi.

Rais wa Ufaransa François Hollande mbele ya Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 25, 2012.
Rais wa Ufaransa François Hollande mbele ya Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 25, 2012. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

"Janga linaloshuhudiwa Syria litakuwa katika historia aibu kwa jumuiya ya kimataifa kama hatutaweza kulidhibiti haraka iwezekanavyo," Bw Hollande amesema, huku akitja eneo la Aleppo (kaskazini mwa Syria) kuwa ni "mji wa kishuja".

Rais François Hollande alizungumzia hasa bila kuitaja, Urusi, mshirika mkuu wa rais Bashar Al-Assad. "Ninawaambia washirika wake wa kigeni, ambaye kila mtu hapa awanajua, kwamba wanapaswa kufikiria amani, la sivyo watabeba mzigo wa lawama na serikali ya Syria kwa kuhusika moja kwa moja katika machafuko yanayoendelea kushuhudiwa nchini Syria," ameonya.

Ufaransa, mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, imeomba taasisi hiyo "kukutana haraka iwezekanavyo" na "kutopumbazika na kauli za baadhi ya viongozi." Hollande ametoa mapendekezo manne katika hali hiyo, ikiwa ni pamoja na "kulazimisha kusitishwa kwa mapigano, kuhakikisha kulinda msafara wa misaada ya kibinadamu kwa walengwa, kuruhusu kuanza kwa mazungumzo ya kisiasa na kuwaadhibu wanaotumia silaha za maangamizi" .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.