Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Watu 26 wauawa katika mapigano katika eneo lenye utajiri wa mafuta

Wapiganaji angalau 26 wameuawa Jumatatu hii katika mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi wa kishia wa Huthi katika hali ya kulidhibiti eneo lenye utajiri wa mafuta mashariki wa mji mkuu wa Yemen, vyanzo vya kijeshi vimebaini.

Vikosi vya jeshi la Yemen vikimshindikiza Makamu rais Ali Muhssien al-Ahmar katika mkoa wa Marib, Agosti 15, 2016.
Vikosi vya jeshi la Yemen vikimshindikiza Makamu rais Ali Muhssien al-Ahmar katika mkoa wa Marib, Agosti 15, 2016. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

"Vikosi vinavyounga mkono serikali vimezindua leo (Jumatatu) operesheni ya kijeshi ili kuudhibiti mji wa Sarwah", chanzo kijeshi kinachounga mkono serikali kimesema, kikimaanisha eneo la mkoa wa Marib linaloshikiliwa bado na waasi wa Huthis ambao wanadhibiti mji mkuu Sanaa tangu Septemba 2014.

Mapigano makali na mashambilizi ya anga ya muungano wa Kiarabu "yamewauawa waasi 16 na wengine kadhaa wamejeruhiwa," chanzo cha kijeshi kimesema.

Askari kumi wanaounga mkono serikali wameuawa na wengine 12 wamejeruhiwa katika mapigano hayo, chanzo hiki kimeongeza.

Kwa mujibu wa vyanzo vingine vya kijeshi, askari wanaounga mkono serikali wamedhibiti milima ya mji wa Sarwah.

Mkoa wa Marib umeendelea kushuhudiwa mapigano makali baina ya vikosi vya tiifu kwa Rais Abd Rabbo Mansour Hadi, anayeungwa mkono na muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi,ambao uko katika vita kwa zaidi ya mwaka mmoja dhidi ya waasi wa Huthi ambao wanadhibiti mji wa Sanaa na sehemu kubwa ya kaskazini.

Saudi Arabia imeongeza mashambulizi ya anga tangu Agosti 9, baada ya kushindwa kwa mazungumzo ya amani nchini Koweit kati ya wadau wote kutoka Yemen.

Aidha, Umoja wa Falme za Kiarabu, moja ya nguzo za muungano wa Kiarabu, umetangaza Jumatatu hii kifo cha askari wake mmoja nchini Yemen, kwa mujibu wa taarifa ya vikosi vya jeshi iliyochapishwa na gazeti la serikali la Emirati WAM.

Machafuko nchini Yemen yamesababisha vifo vya watu karibu 6,600 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.