Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Uturuki yakanusha mkataba wa kusitisha mapigano na Wakurdi

media Jeshi la Uturuki limepiga kambi kwenye milima ya jimbo la Kobane. REUTERS/Umit Bektas

Uturuki imekanusha Jumatano hii kwamba imekubaliana kusitisha mapigano na wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria kwa jitihada za marekani Marekani, ikisema haiwezi "chini ya hali yoyote" kukubali maelewano na "kundi la kigaidi."

"Sisi si hatukubali kwa ya hali yoyote", kinyume na kile "baadhi ya wasemaji wa nchi za nje wanavyosema, maelewano au kusitisha mapigano kati ya Uturuki na wapiganaji wa Kikurdi", amesema Waziri wa mambo ya Ulaya Omer Çelik, kuhusu tangazo lililotolewa Jumanne wiki hii na Marekani.

"Uturuki ni nchi ambayo iko huru na inatambuliwa" , nchi ambayo haiwezi kuelewana na "kundi la kigaidi", ameongeza Waziri Omer Celik akinukuliwa na shirika la Anadolu linalounga mkono serikali ya Uturuki, akimaanisha kwamba chama cha PYD.

Makubaliano ya kusitisha mapigano na chama cha PYD "hayamo vichwani mwetu", Msemaji wa Ofisi ya rais, Ibrahim Kalin, amesema kwenye runinga ya serikali.

Hata hivyo, wakati ambapo serikali ya Uturuki ilitangaza Jumapili kwamba iliwauawa "magaidi 25" wa chama cha YPG, hakuna mashambulizi ya jeshi la Uturuki yaliendeshwa dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi tangu Jumatatu mchana. Makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano yamekua yakibaini kwamba mkataba huo utaanza kutekelezwa toka Jumatatu saa tatu usiku za kimataifa, kwa mujibu wa waasi wa Syria.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana