Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Silaha za kemikali Syria: Paris yaomba vikwazo

Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa umelitaja jeshi la serikali ya Syria na kundi la Islamic State kama walihusika mara nyingi kwa mashambulizi kadhaa ya kemikali yaliyotekelezwa katika miaka ya 2014 na 2015 nchini Syria. Klorini na gesi ya haradali zilitumiwa katika mashambulizi hayo.

Picha iliyopigwa kwa mara ya mwisho mwezi Agosti 2016 ikionyesha uwezekano wa matumizi ya gesi ya klorini katika mji wa Saraqeb, kaskazini mwa Syria.
Picha iliyopigwa kwa mara ya mwisho mwezi Agosti 2016 ikionyesha uwezekano wa matumizi ya gesi ya klorini katika mji wa Saraqeb, kaskazini mwa Syria. Social Media/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza kwa wahusika kuwekwa wazi. Marekani inahitaji wahusika wahukumiwe kwa mujibu wa sheria. Ufaransa inabaini kwamba "Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa kuchukua hatua."

Kulingana na taarifa zetu, Ufaransa inafikiria azimio liwasilishwe mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia uchunguzi wa mashambulizi ya kemikali nchini Syria. Nakala ambayo inaweza, hata hivyo, kukabiliana na kura ya turufu ya Urusi, mshirika wa Assad.

"Katika hali ambapo Syria ni mwanachama wa Shirika linalohusika na kupiga Marufuku ya silaha za kemikali (OPCW) tangu miezi kadhaa, kwa kawaida uchunguzi huu na hitimisho hili, litapelekea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua azimio ambalo ilnaweza na linapaswa kutekeleza idadi ya vikwazo dhidi ya serikali ya Syria, kwani mkataba wa kupiga marufuku silaha za kemikali unatumika kwa mataifa na sio kwa majimbo madogo madogo, " amesema Olivier Lepick, mtafiti msaidizi katika shirika la FRS na mtaalamu wa silaha za kemikali.

Kwa sasa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, amesema amechukizwa kitendo hihi cha utawala wa Bashar al-Assad wa kutumia silaha za kemikali katika mashambulizi mbalimbali.

Na kuhusu mashambulizi ya kemikali yanayohusishwa kundi la Islamic State, Ufaransa imebaini kwamba wanajihadi na utawala wa Bashar al-Assad wanaonekana kuwa kuwaangamaiza raia wa Syria wasio kuwa na hatia.

Kwa upande wa Ufaransa, suala la silaha za kemikali nchini Syria ni nyeti. Mika mitatu iliyopita, shambulizi la gesi ya sarin yaliwaathiri mamia kadhaa ya watu karibu na mji wa Damascus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.