Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Watu 9 wauawa katika shambulizi dhidi ya Chuo Kikuu cha Marekani mjini Kabul

Kwa uchache watu tisa waliuawa katika shambulio dhidi ya Chuo Kikuu cha Marekani katika mji wa Kabul, nchini Afghanistanje, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan.

Mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, unaendelea kukumbwa na visa vya mashambulizi na mauaji.
Mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, unaendelea kukumbwa na visa vya mashambulizi na mauaji. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

"Wanafunzi 7 waliuawa na wengine 30 pamoja na walimu wamejeruhiwa" katika shambulizi dhidi ya Chuo Kikuu cha Marekani katika mji wa kabul Jumatano usiku, Sediq Sediqqi, msemaji wa Wizara ya mambo ya Ndani ameliambia shirika la habri la AFP, akiongeza kuwa polisi wawili pia waliuawa.

Wakati huo huo polisi imefahamisha kwamba operesheni ya kuwasaka washambuliaji imemalizika Alhamisi hii alfajiri baada ya washambuliaji wawili kuuawa, masaa kumi baada ya kuanza kwa operesheni hiyo.

"Tumemaliza kazi yetu. Washambuliaji wawili wameuawa.," Fraidoun Obaidi, mkuu wa polisi mjini Kabul ameliambia shirika la habari la AFP.

Hakuna kundi lililodai mpaka sasa kuhusika na shambulizi, ambalo linakuja wiki mbili baada ya walimu wawili wa chuo kikuu, mmoja kutoka Australia na mwengine raia wa Marekani kutekwa nyara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.