Pata taarifa kuu
PAKISTAN-USALAMA

Pakistan: zaidi ya watu 70 wauawa katika hospitali ya Quetta

Kwa mujibu wa huduma za uokoaji katika eneo la tukio, zaidi ya watu 70 waliuawa na wengine kadhaa walijeruhiwa katika shambulio la bomu lililotokea Jumatatu hii, Agosti 8 dhidi ya hospitali ya mji wa Quetta, mji mkuu wa jimbo linalokabiliwa na hali tete la Balochistan, kusini magharibi, mwa Pakistan.

Mlipuko uliyotokea mbele ya hospitali ya mji wa Quetta, Pakistan, umemewaua watu zaidi ya 70, Agosti 8, 2016.
Mlipuko uliyotokea mbele ya hospitali ya mji wa Quetta, Pakistan, umemewaua watu zaidi ya 70, Agosti 8, 2016. REUTERS/Naseer Ahmed
Matangazo ya kibiashara

Wanajihadi wa kundi la Jumuiya-ul-Ahrar, tawi la kundi la Taliban nchini Pakistan, limekiri kuhusika na shambulio hilo.

Mlipuko huo ulitokea wakati ambapo wanasheria na waandishi wa habari walikua wakikusanyika katika hospitali baada ya kuuawa kwa mwanasheria maarufu, rais wa Chama cha wanasheria katika jimbo la Balushistan, Bilal Anwar Kasi. Miili ilikua imetapaka ardhini katika dimbwi la damu, wakati ambapo watu walionusurika walikuwa wakijaribu kujipa faraja, alishuhudia mwandishi wa habariwa shirika la habri la AFP. Watu waliouawa, wengi wao walikua wameva suti na tai.

"Watu waliouawa ni 70 na 112 waliojeruhiwa," Dr Masoood Nausherwani, Mkuu wa Huduma za Afya katika jimbo la Balochistan, ameviambia vyombo vya habari.

"Mlipuko ulitokea wakati ambapo wanasheria walikua wkikusanyika nje ya idara ya dharura. Baadhi walikuwa ndani, wengine nje ya lango, "amesema daktari mmoja katika Hospitali ya kiraia katikamji wa Quetta, Dk Adnan. "Kulikuwa na mlipuko mkubwa na papo hapo giza lilitanda. Mara ya kwanza nilidhani ni jengo lilillodondoka. Kisha kulikua na kelele, "ameongeza. Wanasheria na waandishi wa habari walikuwa wamekusanyika baada ya kuuawa kwa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria katika jimbo la Balushistan, Bilal Anwar Kasi.

Tawi la kundi la Taliban nchini Pakistan lakiri

Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif amelaani shambulizi hilo na kuamuru hatua mpya za kiusalama. "Hatutokubali mtu yeyote kuvuruga amani katika jimbo ambako hali ya usalam imerejeshwa baada ya kujitolea kwa vikosi vya usalama, polisi na raia," Bw Sharif amesema kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi yake.

Shambulizi hili limedaiwa kutekelezwa na kundi la Jumuiya-ul-Ahrar, ambalo ni tawi la kundi laTaliban nchini Pakistan. Kundi hili, katika siku za nyuma, lilidai kutekeleza mashambulizi ambayo halijawahi kutekeleza. "Tehreek-e-Taliban Pakistan Jumuiya-ur-Ahrar (JA-TTP) ladai kutekeleza shambulizi hilo na linaahidi kuendelea kuongoza aina ya shambulio hilo. Hivi karibuni tutarusha video kuhusu shambulio hilo, " msemaji kundi hilo, Ehsanullah Ehsan, amesema katika taarifa yake.

Jimbo la Baluchistan, lililo kwenye mpaka wa Iran na Afghanistan, ni jimbo lenye utajiri wa mafuta na gesi, ambalo linakabiliwa na vita vya kidini baina ya Wasunni na Washia, mashambulizi ya wanamgambo wa Kiislamu na waasi waliojitenga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.