Pata taarifa kuu
IRAQ-IS

Wapiganaji wa kundi la IS watimuliwa Fallujah

Vikosi vya Iraq vimeudhibiti karibu mkoa wote wa Falluja, ambapo kundi la Islamic State (IS) linaonekana tu katika maeneo mawili ya kaskazini mwa mji yanayopatikana magharibi mwa mji wa Baghdad, afisa mmoja wa jeshi amesema Jumatano hii.

Jeshi la Iraq limeanzisha operesheni Jumatatu hii Mei 23, 2016kwa lengo la kudhibiti mji wa Falluja kiutoka mikononi mwa kundi la IS
Jeshi la Iraq limeanzisha operesheni Jumatatu hii Mei 23, 2016kwa lengo la kudhibiti mji wa Falluja kiutoka mikononi mwa kundi la IS AHMAD AL-RUBAYE / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kundi la Islamic State limetimuliwa kaskazini na katikati ya mkoa wa Fallujah", Abdulwahab al-Saadi ameliambia shirika la habri la AFP. "Wanabaki tu wapiganaji wa kundi la Is katikamaeno ya Al-Mouallemine na al-Jolan kaskazini mwa Iraq", afisa hyo wa jeshi ameongeza

"katika eneo la A Al-Jolan, wamejidhatiti vilivyo lakini tumekua tukijaribu kuwatimu na tuliua idadi kubwa ya wapiganaji wa kundi hili," alisema.

Vikosi mashuhuri dhidi ya ugaidi (CTS), polisi na vitengo vingine vya kijeshi viko kwenye mstari wa mbele katika mashambulizi hayo yaliyoanzishwa Mei 23 kwa lengo la kuweka kwenye himaya yao mkoa wa Falluja, kutoka mikononi mwa wanajihadi wanaoushikilia tangu Januari 2014.

Waziri Mkuu Haider al-Abadi alisema wiki iliyopita kwamba waliitwa ngome ya wanajihadi ilioko kilomita hamsini magharibi mwa mji wa Baghdad. Robo tatu ya mji iko chini ya udhibiti wao, kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu jeshini, jenerali wa na maafisa wengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.