Pata taarifa kuu
UTURUKI-USALAMA

Kituo cha polisi chashambuliwa kusini mashariki mwa Uturuki

Shambulio la bomu la kutegwa ardhini likilenga Jumatano hii kituo cha polisi katika eneo la Midyat kusini mashariki mwa Uturuki, siku moja baada ya shambulio kama hilo lililotokea katika jiji la Istanbul.

Bomu llilotegwa ndani ya gari, Mei 1, 2016, mbele ya kituo cha polisi cha Gaziantep, Uturuki.
Bomu llilotegwa ndani ya gari, Mei 1, 2016, mbele ya kituo cha polisi cha Gaziantep, Uturuki. Ihlas News Agency via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo liligharimu maisha ya watu 11, na kuwajeruhi wngine 36, shirika la habari linalounga mkono serikali la Anatolia.

Mlipuko mkubwa ulitokea nje ya jengo katika mji huo wa mkoa wa Mardin na magari ya wagonjwa yametumwa katika eneo la tukio, shirika hilo la habari limeongeza, na kuwahusisha waasi wa Kikurdi na shambulio hilo.

Hata hivyo waasi wa Kikurdi hawajazungumza lolote kuhusu shambulio hilo. Watu wengi wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.